Soko liko wapi

Soko liko wapi
Soko la Mazao ya wakulima ndiyo changamoto kubwa huko vijijini. Wakulima wakisubiri wateja kando ya barabara ya Morogoro-Dodoma eneo la Gairo ili wanunue viazi vitamu

Special News Pages

Saturday, July 3, 2010

Family Planning

MAKALA AFYA YA JAMII


WANAOATHIRIWA NA NJIA ZA KISASA ZA KUPANGA UZAZI, WENGI WAO HUTUMIA KABLA YA KUONANA NA WATAALAMU.

Na Hassan Simba, Aliyekuwa Turiani.

KATIKA kipindi cha kisichopungua miaka 30 sasa wanaume na hasa wanawake wamekauwa wakitumia njia mbalimbali za kisasa kupanga uzazi, hii imetokana na hamasa kubwa inayofanywa na serikali na asasi nyingine za kijamii zilizo na lengo la kuleta mbadiliko chanya.

Matumizi haya ya njia za kupanga uzazi si kitu kipya kwa jamii ya watnzania kwani hapo nyuma wazee wetu waliweza kupanga uzazi ka kutumia njia za asilia ambazo kwa sasa zinaonekana kutoweza kufaa zidi kutokana na mabadiliko ya kisayansi na kimazingira, nandio maana njia hizi za kisasa zimekuw zikitumika zaidi.

Njia za kupanga uzazi za kisasa ni pamoja na vidonge, mipira ya kiume na kike, kitanzi, sindano, vipandikizi, lakini zipo njia za kudumu za muda mrefu ambazo ni kwa kufanya upasuaji mdogo usiohitaji nusu kaputi kwa mama au baba.

Kwa mujibu wa sensa ya idadi ya wtu na makazi ya mwka 2002 inadhihirisha kwamba idadi ya watu nchini Tanzania imeongezeka kutoka watu milioni 23.1 1988 hadi milioni 34.4 mwaka 2002, makisio ya ongezeko la idadi ya watu yanonesha kwamba nchi yetu ina wtu milioni 39.4 hadi mwaka 2008 na inatarajiwa itaongezeka hadi kufikia wtu milioni 63.5 mwaka 2025 hii ndiokusema kuwa ongezeko la idadi ya watu linakuwa kwa kiwango cha 2.9 kwa mwaka.

Waataalamu wa uchumi wanasema kuw upo uhusiano mkubwa kati ya kukua kwa uchumi na ongezeko la idadi ya watu, katika hili no wanaungana na wataalamu wa masula ya afya kuhimiz jamii ikubaliane na kujiunga katika uzazi wa mpango.

Kuongezeka kwa idadi ya watu kwa kasi huku miundombinu ya uchumi ikiw ileile isiyoweza kuhimili ongezeko hilo ni wazi kuwa ukuji wa uchumi utasuasua huku huduma za kijamii nazo zikiendelea kuwa duni.

Inaelezwa kuwa kupungua kwa kasi ya ongezeko la idadi ya watu kunatoa fursa ya kuonezeka kwa kiwango cha kukua kwa uchumi, lakini pia kupungua kwa haraka kwa kiwango cha kuzaana katika ngazi ya taifa, kunatoa fursa kwa familia nyingi kuondokana na umasikini

Lakini pia kuongezeka kwa kasi ya kuzaana kunaibua matatizo mengine ikiwa ni pamoja na kukosekan kwa huduma bora za afya ya uzazi kutokana na uchache wa wataalamu na na ufinyu wa miundombinu tuliyonayo.

Inaelezwa kuwa ni asilimia chache kati ya kinamama waliona uwezo w kuzaa ambao wamefikiwa na huduma bora za afya ya uzazi na matokeo yake ni kuwapo kwa vifo vingi vya wkinamma kabla na wakati w kujifungua ambapo kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO wakinamama 578 kati ya 100,000 wnakufa kila mwaka kutokana na matatizo ya uzazi.

Kutokana na sababu hizo na nyingine nyigi ambazo zijzitaja hapa, kumepelekea kuwapo kwa onezeko la maumizi ya njia za kupanga uzazi ili kuendendana na hali hali ya kiuchumi ulivyo sas hapa nchini, ambapo katika hili wadau mbalimbali wamekuw wkishirikian n serikali kuhakikish hilo linafnikiw.

Lakini pamoja na kuwapo kwa muitikio mkubwa wa jamii kutumia njia hizo kwa hiyari, kumekuwepo na changamoto nyingi katika utekelezaji wake ikiwa ni pamoja na kudaiwa kuwa njia hizo karibu zote zina madhala kwa mtumia hali inayowafanya walikwishaanza ama kuachana nayo au kujaribu nyingine.

Amina Haji ni Mkunga wa jadi kutoka katika kijiji cha Kwadori kata ya Diongoya wilayani Mvomero Mkoa wa Morogoro, katika mahojiano na mwandishi w makala haya aliyetembelea kijiji hicho hivi karibuni, anasema kuwa alianza kufanya kazi hiyo tangu mwaka 1990, na kusema kuwa amekuwa akiwashauri wateja wake kutumia njia ya uzazi wa mpango ya asili.

Mama huyu wa makamo anasema kuw amekuw akifanya hivyo baad ya zile z kisasa kuonekana kuwa na madhara mengi yanayosababisha wengi wa wkinamama kijijii hapo kutopenda kuenelea kuumia.

Anasema njia hiyo ilikuwa ikitumiwa na wataalam wa tiba ya asili kwa kuchukua mti aina ya “Masaraka” ambao hupatikana hasa katika maeneo ya mbugani na kuyetengeneza vizuri kisha kuyatunga kwa kuchanganya na shanga na mwanamke mwenye mtoto mchanga kuvaa kiunoni.

Katika kipindi hicho cha kulea mtoto mwanamke huwa hatakiwi kukutana na mwanaume kwa ajili ya kujiepusha na kupata mimba akiwa na mtoto mdogo hali ambayo inaweza kudhoofisha afya ya mtoto iwapo hatabaini mapema kama amepata mimba.

Lakini njia hiyo nayo inaonekana pia inaweza kuleta madhara kwa mujibu wa imni ya wtumiaji kuwa iwapo mwanamke ataitumia katika nyumba yake huathiri hata mifugo kama kuku ndani ya nyumba kwa kipindi hicho hawataweza kutaga mayai.

Monika Kibwilo ni mkunga wa jadi wa kabila la wanguu anasema njia hiyo ya uzazi wa mpango ya asili ilikuwa ikitumiwa na jamii ya kabila hilo lakini kwa kiasi kidogo kwani wanawake walio wengi walikuwa wakitumia njia ya kuzuia kupata mimba kwa kutengana na wanaume wao katika kipindi wanacholea watoto hadi pale wanapokuwa wakubwa.

Anasema njia hiyo pamoja na kwamba ni nzuri kwa upande fulani lakini ina matatizo kwani wanamke anatakiwa kuwa makini sana katika kuilinda dawa hiyo kwani iwapo itapotea kama kubebwa na panya inaweza kupelekea mwanamke asizae tena katika maisha yake yote.

Imani hiyo ilisababisha wanawake walio wengine kuogopa kutumia njia hiyo na kuwafanya kutumia zaidi njia ya kutengana na wanaume zao wanapokuwa katika kipindi cha kulea watoto wadogo.

Aisha Hassan mkazi wa kijiji cha Lusanya kata ya Mtibwa mwenye anasema kuwa alipopa motto wake wa nne aliamua kuanza kupanga uzazi ili aweze kupata muda wa kushiriki katika shughuli za kuzalish kipato kwa familia.

Anasema njia aliyoichagua ilikuwa ni vidonge ambavyo aliviagizia kwa mdogo wake nayeishi Morogoro mjini, kutokana na kuwa havipatikani kijiji hapo, lakini pia hkuwa amekubaliana na menzawake juu ya uamuzi huo.

Lakini Aish nakiri kuw alishuriwa na jirani yake ambaye lishwhi kutumia njia nyingi kadhaa lakini zilimlete madhar makubwa na ndipo alipoamua kutumia vidonge na hivyo hata yeye alipotaka kutumia lichagua njia hiyo.

“Lakini nona ninmbadiliko mengi katika mwili wngu tangu nilipoanza kutumia vidonge hivi…….siku zangu za mwezi zinaingia bila kuwa na mpangilio maaluumu na ninkonda sana..huu sio mwili wangu kabisa….nafikiria kuachananayo” Anasema dada huyu anayeonesha kukata tama.

Mwanamke mwingine aitwaye Sabithina Athumani ni mmoja kati ya wanawake wanaodai kuathirika na dawa za uzazi wa mango ambaye anasema alianza kwa vidonge, sindano na baadae vipandikizi lakini sasa ameamua kuacha kabisa kutokana na matokeo aliyoyaita kuwa mabaya.

“Nilainza kwa vidonge lakini kusema ukweli vilinishinda kwa kuwa mimi ni mkulima, mara nyingi nilikuwa nikisahau kumeza hasa kwa kuwa huwa nakuwa nimechoka, uzembe huu ulinipelekea nikapata mamba mbayo sikuipanga,

Nikaona bora nichome sindano lakini haikunifaa kwani nilikuwa nikipata siku zangu mfululizo tena zikimwagika kwa wingi, nilibadilishiwa kwa kuwekwa vipandikizi,

Mariam Omari anasema katika maisha yake alifanikiwa kuzaa watoto watano na kila mtoto alikuwa akipa katika ipindi cha mwak mmoja tangu yule aliyetangulia kuzaliwa, mwishoe alimua kuanza ktumia njia za kupang uzazi ili kupat motto kila bada ya miaka mitatu au zaidi baada ya mwingine.

“Nilipoamua kuanza kutumia njia za kupanga zazi nilimuuliza mama mmoja ambaye niliambiwa anatumia njia hizo ambaye naye alinishuri nitumie vidonge na nikaanza kutumia, lakini tangu nilipoanza sijapata siku zangu…….yani sijui hata la kufanya naweza kutumika kwa dakika chache na ikikatika basi hadi mwezi mwingine au nisione kabisa”, anasema Mama huyu mwenye mwili mkubwa asioumudu vyema.

Wakinamama hawa ni mfano w wakinamama wengi karibu kona zote za nchi yetu hasavijijini ambao wmekuw wkiumia njia hizi z kupanga uzazi bila ya kupata ushuri wa kitaalamu kutoka kwa maafisa wa tiba katika maeneo yao, na matokeo yake ni kuleta madhara ambayo kama wangeshauriwa kabla ya kuanza kutuia yngetokea.

Dk. Godfrey Mapunda, ni mtaalamu wa afya ya uzazi anayefanya kazi katika shirika lisilo la kiserikali la EngenderHealth mradi wa ACQUIRE Tanzania kanda ya Morogoro na mbao unafadhiliwa na shirika la misaada la Marekani USAID, nasema kuwa utafiti umeonesha kuwa wakinamama wengu wanaanza kutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango kwa kushauriwa na majirani zao wasio na utaalamu.

Anasema matokeo ni kupata madhara muda mfupi mara baada ya kuanza kutumia hali ambayo inapelekea wengi wao kuamua kuacha kabisa au kutumia njia nyingine ambayo nayo inakuwa ni kubahatisha na hivyo kuwapo kwa uwezekano kubwa wa njia hizo mbadala kumletea madhara pia.

“Sisi wataalamu tunashuri kabla mama hajanza kutumia nji hizi kwanza aonane na mtaalam wa tiba ili kumfanyia uchunguzi na kasha kumshuri ni njia ipi atumie na ambayo haitalete madhara…..huezi kukurupuka na kuanza kutumia vidonge wkti unaupungufu wa damu lazima itakusumubua tu” anasema mtaalamu huyu.

Mtaalamu huyu anasema kuwa upo uhusiano mkubwa kti ya mdhr wanayoyapata wakinamama wnaotumia njia hizo za uzazi wa mpango bila ya kupata ushauri wa kitaalamu na madhara yatokanyo na matumizi hayo.

Dk. Mapunda anasema kuwa mama ni lazima apimwe wingi wa damu kbla ya kumshauri kutumia vidonge vinginevyo vitazidi kumkusha na atakonda na huku afya yake ikiendelea kudumaa, hali ambayo ndiyo inayolalamikiwa sana watumiaji wengi wa vidonge.

Anasema huwezi kumshauri mama kutumia njia ya kitanzi kabla ya kumpima na kujua kama anamagonjwa ya siri kama vile gono au kawende kwani iwapo njia hii itatumika kwa mama mwenye mambukizi haitaweza kufanya kazi na matokeo anapata mamba licha ya kwekew kitanzi.

“Unaweza usijue ni kwanini mtaalamu anakutaka upimwe kwanza damu au mkojo kabla ya kukushauri utumie njia gain ya uzazi wa mpango……lakini unapoamua kutumia kwa kushuriw vichochoroni hakika uwezekano wa kupata madhara ni mkubwa sana….tabia hii inapaswa kuachwa mara moja ili kunusuru afya za wakinamama hawa”anasema Mapunda.

Anasema ni lazima jamii ikafahamu uhumuhimu wa kutumia njia za uzazi wa mpango kwani kuna uhusiano na kuongezeka kwa vifo vya wakinamama na miamba zisizohitajika,kuhalibika mamba na matatizo kadhaa yatokanayo na ujauzito kw wkinamama wengi hapa nchini.

Mtaalamu huyu aliyebobea katika masula y fya ya uzazi anasema kuwa kutumia njia za uzazi wa mpango kunapunguza vifo vya wakinamama kwa asilimia kati ya 25 na 30, hivyo ni muhimu jamii ikalitambua hili.

Mapunda anawaambia waandishi wa habari kutoka mikoa ya kanda ya mashariki waliokuwa wakifanya utafiti juu ya afya ya uzazi katika wilaya ya Mvomero, kuwa elimu zidi inahitajika kwa jamii juu ya umuhimu wa kumuona mtaalamu kwanza kabla ya mama hajaanza kutumia njia za uzazi wa mpango vinginevyo wataendelea kuamini dhana potofu kuwa njia hizo zinamadhara makubwa kuliko faida.

Anasema shirika lake limekuwa likisisitiza zaidi njia za kupanga uzazi za kudumu ambazo zina faida nyingi kwa jamii, kama vile upunguza msongamano kliniki z uzazi wa mpango, ni tendo la mara moja kwa faida ya miaka mingi, huongeza hamu ya tendo la ndoa,mama hupata muda wa kujishughulisha n kazi za uzalishaji kwani haendi tena kliniki.

“Njia hizi zipo za aina mbili ambazo ni kufunga uzazi ndani ya siku saba baada ya mama kujifungua…pili ni kufunga uzazi ambako hakuna uhusiano na ujauzito….ni upasuaji rahisi ambao hautumii nusu kaputi lakini pia mteja hufanyiwa na kurudi nyumbani siku ileile” anasema Mapunda.

Lakini wakati mtalamu huyu antoa ushauri huo bado kuna changamoto nyingi juu ya kufikiwa kwa huduma za kitaalamu hasa kwa wakinamam wisho vijijini, wanawez kusikia hili na kuamua kufuata ushauri huo je wanapata wataalamu karibu na maeneo wanayoishi, hili ni swli ambalo majibu yke hayawezi kuwa rahisi kama ambavyo wkinamama hawa wangependa iwe.

Dk Mashaka Shemkande ni kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Misheni ya Turiani (Bwagala ) anasema hospitali hiyo ilianzishwa mwaka 1962 ikilenga kuhudumia vijiji vitano vinavyoizunguka ambavyo ni Diongoya, Digalama, Kisdala, Manyinga na Madizini katika tarafa ya Turiani.
Lakini sasa hospitali hiyo imekuwa ikiwahudumia watu wengi zaidi ya mara tatu ya lengo hali inayoifanya kuhelemewa has ikizingatiwa kuwa rasilimali zilizowekezwa wakati huo hazikulenga kuhudumia idadi kubwa y watu kama ilivyo sas.

“Hospitali hiyo awali ilikuwa ikihudumia wagonjwa takribani 18,000 lakini kwa sasa idadi hiyo kwa sasa imeongezeka kwa zaidi ya mara tatu..hili ni ongezeko kubwa na hasa ikizingatiwa kuwa uwezo wake bdo ni uleule wa 1962” Anasema Mtaalamu huyu wa tiba.

Anasema katika mwaka huu kuanzia Januari hadi Mei wakina mama waliojifungua katika hospitali hiyo ni 1226 na kwamba robo kati yao ni wle ambao umri wao haushariwi kubeba mamba na hivyo kuwa katika wakati mgumu wa kukabiliwa na matatizo mengi ya uzazi.

Kati ya akina mama hao waliojifungulia hospitalini hapo sita walipoteza maisha na kati ya hao wawili ni walio katika umri ambao hawakutakiwa kuanza kuzaa na kuitaja hiyo kuwa ni sababu kubwa inayochangia vifo hivyo.

Anasema tatizo la mimba katika umri mdogo katika wilaya ni kubwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo wanafunzi kukosa elimu sahihi ya afya ya uzazi sambamba na umaskini katika jamii

“Unajua wilaya hii haina hospitali wote wanategeme hapa nah ii ni ya Misheni madheebu ya Roma haturuhusu kbisa mambo ya uzazi wa mpango..kwahiyo hata kupata ushauri wa masuala hayo hapa ni vigumu na kwakuwa hakuna maali pengine karibu wanajikuta wakiingia katika matatizo” anasema Shemkande..

Hata hivyo anasema hospitali hiyo inakabiliwa na tatizo la watumishi wa huduma za afya kutokana na waliopo kwa sasa maafisa tabibu wapo wanne na mahitaji ni kati ya 11 na 12 huku waguuzi watakiwa 60 lakini waliopo ni 34,madaktari watatu na mahitaji angalau watano na madaktari bingwa hakuna na wamekuwa wakitegemea kutoka KCMC na AMREF.

MWISHO.

No comments:

Post a Comment