Above: a 12 year old girl, at Turiani Hospital, Morogoro, at labour ward waiting for her turn to deliver. Above left: An 18 year old secondary school girl given money donation from journalists to get operation on her breast absess. Below: A 13 year old girl breat-feeding her baby, a product of rape. She lives in Bariadi, SImiwi Region. Tanzania
Mimba za Utotoni kwa sasa limekuwa kama ugonjwa wa kuambukiza. Ingawa baadhi ya maeneo tatizo hili linanekana lakini kuna maeneo mengine, hasa vijijni, tatizo hili limekuwa kubwa na linaonekana kukosa dawa ya kuliponyesha kabisa.
Wasichana wa umri mdogo wanapata mimba kutoka kwa watu wazima na wengine wanapewa na watoto wenzao. Vyanzo vikubwa ni umasikini wa watoto na wazazi, na kukosa elimu ya kutosha kuhusiana na elimu ya afya ya uzazi na kupata ujuzi wa stadi za maisha zitakazoweza kuzuia vishawishi.
Wazazi na shule wanapaswa kubadilisha mfumo wao wa kuelimisha na kulinda watoto na kujifunza mahitaji ya mazingira mapya kwa watot. Mazingira haya ni pamoja na kuwa rahisi kwao kupata taarifa kutoka televisheni, radio, magazeti na majarida, intaneti au simu bila kuingiliwa na wazazi, walezi au walimu.
Rural Infonews Network inashauri kuwa wadau wote katika suala hili, ikiongozwa na idara au wizara husika za serikali, watafute njia mwafaka za kutatua tatizo hilo. Aidha nadhani huu ni wakati mwafaka vile vile wa kushirikisha vyombo vya habari ili vitumike kama nyenzo za mabadiliko ya kitabia miongoni mwa vijana na watu wazima pia.